WINGA ARJEN ROBBEN AMMIMINIA SIFA LOUIS VAN GAAL



WINGA ARJEN ROBBEN AMMIMINIA SIFA LOUIS VAN GAAL
WINGA Arjen Robben ni kama kammwagia sifa kocha wao wa zamani, Louis Van Gaal bada ya kusema kuwa mafanikio waliyonayo hadi sasa yametokana na Mholanzi huyo na huku akimtaka kocha wao mpya, Carlo Ancelotti akijenge kikosi hicho kama walivyokuwa watangulizi wake, Jupp Heynckes na Pep Guardiola.

Van Gaal alikuwa kiongozi wa klabu hiyo ya Allianz Arena kati ya mwaka 2009 na 2011 na aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya Bundesliga na DFB-Pokal mwaka 2009-2010.

Mbali na huyo, Heynckes aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi ya ndani ya mabingwa Ulaya mwaka 2013 kabla ya kumkabidhi mikoba Guardiola ambaye alitwaa mataji matatu ya Bundesliga kabla ya kuhamia Manchester City.


Kutokana na hali hiyo, winga huyo anaamini mabao yataendelea kuwa hivyo wakati Ancelotti atakapotua kwenye klabu hiyo ya Allianz Arena.


Comments