VAN PERSIE ANUKIA LIGI KUU ENGLAND... huenda akarejeshwa premier na Crystal Palace, West ham zinazomwania
STAA Robin Van Persie huenda akarejea katika michuano ya Ligi Kuu England majira ya msimu wa joto baada ya timu za Crystal Palace na Westham kutuma ofa ya kumtaka.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Arsenal anasemekana kuwa anatamani sana kurejea England ikiwa ni msimu mmoja tangu awachezee vinara wa Uturuki, Fenerbahce.
Wakala wa staa huyo anadaiwa kuwa ameshamtafutia klabu kadhaa Ulaya, lakini Mholanzi huyo anasemekana mawazo yake ni kurejea London akiwa na familia yake.
Comments
Post a Comment