USHINDI MWINGINE WA GENK YA SAMATTA WAIWEKA PAZURI EUROPA LEAGUE


USHINDI MWINGINE WA GENK YA SAMATTA WAIWEKA PAZURI EUROPA LEAGUE

Genk

Klabu ya KRC Genk ya Belgium anakokipiga mtanzania Mbwana Samatta, imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Cork City katika mchezo wa kwanza wa raundi ya tatu kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Europa League.

Bao pekee katika mchezo huo limefungwa na Leon Bailey dakika ya 31 kipindi cha kwanza baada ya kuachia kiki kali akiwa nje ya eneo la box na shuti hilo kuzama moja kwa moja wavuni.

Mbwana Samatta ambaye alicheza dakika zote za mchezo huo, alipiga shuti la mbali dakika za lala salama kabla ya Bailey pia kuachia shuti kali lakini juhudi za McNulty golikipa wa Cork City zilizima ndoto za Genk kupata goli jingine.

Usiku wa Alhamisi ijayo timu hizo zitarudiana ili kumpata mshindi atakayesonga mbele kwenye hatua inayofuata.



Comments