USAJILI WA SADIO MANE, GEORGINIO WIJNALDUM NDANI YA LIVERPOOL WAMKUNA FILIPE COUTINHO



USAJILI WA SADIO MANE, GEORGINIO WIJNALDUM NDANI YA LIVERPOOL WAMKUNA FILIPE COUTINHO
STAA Filippe Coutinho ameelezea kuridhishwa na nyota waliosajiliwa na Liverpool, Sadio Mane na Georginio Wijnaldum na anasema kuwa anavyoamini ni wepesi na wenye kasi.

Mane na Wijnaldum hivi karibuni walisaini mkataba wac muda mrefu na klabu hiyo ya Anfiled na hivyo kuwa nyongeza mpya kenye kikosi cha kocha Jurgen Klopp kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu England.

Kutokana na hilo, Coutinho alisema juzi kwamba anaridhika na kile ambacho mastaa hao wameongeza katika timu, hususan utoaji wao wa pasi.

"Ninachokitazama ni kwamba nitacheza nao. Wote wawili ni wachezaji wazuri na wepesi na hivyo ukiwapigia mipira mirefu wanaweza kukimbilia na kuifikia," aliongeza nyota huyo.


Hata hivyo, alisema kwamba katika kikosi hicho si wachezaji hao wawili tu ndio wazuri bali kuna wengine wengi ambao anaamini atafanya nao kazi vizuri.


Comments