RIPOTI ya uchunguzi wa matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku kwenye timu ya wanamichezo ya Urusi iliyoshiriki mashindano ya Olimpiki mwaka 2014 huenda ikaizuia timu hiyo kushiriki mashindano haya yatakayofanyika nchini Brazil.
Tume huru ya uchunguzi iliyoundwa na taasisi ya dunia ya kupambana na matumizi ya dawa haramu michezoni (Wada), ilifanya upelelezi wake na itauweka wazi siku ya Jumatatu.
Mashindano ya Olimpiki yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 5, mwaka huu na tayari wanariadha wa kuruka viunzi wa Urusi wameondolewa kabla ya mashindano kuanza.
Comments
Post a Comment