UJERUMANI imekosa            penalti tatu katika hatua ya mikwaju ya penalti kwenye mchezeo            wa robo fainali dhidi ya Italia, lakini bado wakashinda na            kutinga nusu fainali ya Euro 2016.
        Timu hizo            zilikwenda sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 na ilipofika hatua            ya mikwaju ya penalti Ujerumani wakashinda 6-5.
        Miamba hiyo ya soka            barani Ulaya ililazimika kwenda hadi penalti ya tisa ndipo            mshindi alipopatikana kwa Italia kupoteza jumla ya penalti nne            huku Ujerumani wakipoteza tatu.
        Ujerumani walipata            bao la kuongoza dakika ya 65 kupitia kwa Mesut Ozil            lakini Leonardo Bonucci akaisawazishia Italia kwa njia ya            penalti dakika ya 78. 
                 Hivi ndivyo            penalti zilivyopigwa
        Jonas Hector              akishangilia penalti yake iliyoipa Ujerumani ushindi dhidi              ya Italia
        Hector akishangiliwa na              wenzake
        Italia hoi
        Matteo Darmian akikosa              penalti
        
Comments
Post a Comment