Wenyeji wa michuano ya Euro 2016 - Ufaransa wametinga hatua ya nusu fainali kwa kishindo baada ya kuitandika Iceland 5-2.
Iceland iliyoing'oa England katika hatua ya mtoano, ilishindwa kabisa kufurukuta na kujikuta ikienda mapumziko ikiwa nyuma kwa bao 4-0 kwa magoli yalifungwa na Olivier Giroud, Paul Pogba, Dimitri Payet na Antoine Griezmann katika dakika ya 12, 19, 43 na 45.
Kipindi cha pili Iceland walipata bao kupitia kwa Kolbeinn Sigthorsson kunako dakika ya 56 kabla Olivier Giroud hajaifungia Ufaransa bao la tano dakika ya 56 huku Birkir Bjarnason akiipa bao la pili Iceland dakika ya 84.
France (4-2-3-1): Lloris 7; Sagna 7, Umtiti 6, Koscielny 6 (Mangala 72, 6) Evra 6.5; Pogba 7, Matuidi 7.5; Sissoko 6.5, Griezmann 7.5, Payet 7.5 (Coman 80); Giroud 8 (Gignac 60, 6.5).
Iceland (4-4-2): Halldorsson 6; Saevarsson 6, Arnason 5.5 (Ingason 46, 6), R Sigurdsson 5.5, Skulason 6; Gudmundsson 6, Gunnarsson 5.5, G Sigurdsson 6, B Bjarnason 5.5; Sigthorsson 5.5 (Gudjohnsen 83), Bodvarsson 5.5 (Finnbogason 46, 6).
Olivier Giroud akishangilia moja ya mabao yake mawili
Giroud akiifungia Ufaransa kwa guu la kushoto dakika ya 12
Ilikuwa ni siku njema kwa Giroud
Wachezaji wa Ufaransa wakikimbia kumpongeza Giroud
Comments
Post a Comment