UONGOZI wa Arsenal umekubali maombi ya mashabiki ya kumpa timu hiyo nahodha wao wa zamani, Tony Adams.
Mlinzi huyo ambaye pia alikuwa nahodha wa England, aliichezea kwa mafanikio Arsenal katika mechi 504 kati ya mwaka 1983-2002 akifunga mabao 32 na kutwaa mataji kibao.
Mashabiki wanasema kwavile Tony Adam anaujua vema utamaduni wa klabu hiyo iliyomkuza, ndie pekee mwenye uwezo wa kuipa mafanikio na mataji zaidi ya waliyoyapata kutoka kwa Wenger.
Uongozi umeridhia Adam afanye kazi ya kumsaidia Wenger ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake wa sasa ili atakapopewa timu asiwe mgeni nayo.

Comments
Post a Comment