STRAIKA MICHY BATSHUAYI MBIONI KUTUA CHELSEA



STRAIKA MICHY BATSHUAYI MBIONI KUTUA CHELSEA
STRAIKA Michy Batshuayi yuko mbioni kutua katika klabu ya Chelsea baada ya kufuzu vipimo vya afya jijini Bordeaux, kwa mtandao wa Sky Sports.

Batshuayi aliye kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Ubelgiji kwenye michuano ya mataifa ya Ulaya "Euro 2016", amekuwa akihusishwa na klabu kubwa Ulaya baada ya kufunga mabao 17 akiwa Marseille msimu uliopita.


Mshambuliaji huyo alipewa ruhusa kufanya vipimo na kocha wake katika timu ya taifa kwa ajili ya kukutana na timu ya madaktari wa Chelsea kwa ajili ya kukamilisha uhamisho utakaogharimu pauni mil 33.


Comments