KIUNGO mahiri na nahodha wa zamani wa England, Steven Gerrard, anatazamiwa kupewa mikoba ya kuinoa timu ya taifa ya vijana ya England, baada ya mazungumzo na mwenyekiti wa chama cha soka nchini humo, Martin Glenn.
Imeripotiwa kuwa, Glenn amekuwa na mazungumzo na nyota huyo wa zamani wa Liverpool kwa ajili ya kumkabidhi jukumu hilo, kutokana na kuwa na beji ya ukocha ngazi ya UEFA pamoja na mafanikio aliyoyapata kama nahodha.
Hata hivyo, hiyo imetafsiriwa kuwa anaandaliwa mazingira ya kuchukua nafasi ya Roy Hodgson katika kikosi cha wakubwa, baada ya kujiuzuru kufuatia kuondolewa kwenye michuano ya Euro 2016 inayoendelea nchini Ufaransa.
Msululu unazidi kuongezeka wa nani achukue mikoba ya Hodgson ambapo mbali ya Gerrard, pia Arsene Wenger na Jurgen Klismann wote wanahusishwa kumrithi.
Comments
Post a Comment