WAKATI ambapo dirisha la usajili wa majira ya joto limeanza, straika Saido Berahino amethibitisha ataendelea kubaki kukipiga katika kikosi cha West Bromwich Albion.
Msimamo wa Berahino unakuja baada ya kuwepo kwa tetesi kuwa alikuwa anajiandaa kujiunga na Tottenham Hotspur, huku akitajwa pia kutakiwa na Newcastle United.
Barahino alijiunga na Spurs katika usajili wa majira ya joto lakini hakuwahi kupata mafanikio katika kikosi kilichokuwa chini ya Tony Pulis.
Kwa mujibu wa Pulis, straika huyo hakuwa chaguo la kuwemo katika kikosi cha kwanza, hivyo aliamua kutimkia West Bromwich Albion.
Hata hivyo, kiwango cha straika huyo mwenye umri wa miaka 22, kimemrejesha kwenye mawindo ya timu nyingi za premier ambapo Newcastle tayari iliweka mezani dau la pauni mil 24.
Berahino amenukuliwa akisema: "Nimeamua kubakia hapa kwa sababu nimekuwa na mafanikio kuliko nilivyokuwa Spur."
"Nimejipanga kwa ajili ya kuendelea kupandisha kiwango kwasababu nina nafasi ya kufanya hivyo, kwakuwa nina uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza."
"Hii ni faraja kwa kila mchezaji kuona anapata nafasi ya kucheza. Thamani ya kila mtu ni kuona anaaminiwa na kocha wa timu yake. Mimi ni miongoni mwa wanaoaminiwa hapa," alisisitiza Berahino.
Berahino msimu huu amepachika mabao sita akiwa na Bromwich, huku akiweka rekodi ya kufunga jumla ya mabao 22 katika mechi za mashindano yote.

Comments
Post a Comment