Sentahafu wa Ureno Pepe amerejea katika mazoezi kamili kujiandaa na mchezo wa fainali ya Euro 2016 dhidi ya wenyeji Ufaransa utakaochezwa Jumapili.
Pepe ambaye pia ni sentahafu wa Real Madrid aliukosa mchezo wa ushindi wa 2-0 katika nusu fainali dhidi ya Wales baada ya kuumia paja kwenye mechi ya robo fainali iliyowakutanisha na Poland.
Beki huyo alifanya mazoezi ya peke yake Alhamisi na Ijumaa lakini Jumamosi akaungana na wachezaji wenzake kufanya mazoezi ya pamoja na sasa anatarajiwa kuanza katika mtanange wa fainali.
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo ameweka wazi kuwa amefurahishwa na kurejea kwa Pepe na kusema anaamini beki huyo kisiki atachagiza ushindi siku ya Jumapili.
Sentahafu wa Real Madrid Pepe amerejea kundini
Nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo anaamini Pepe atachagiza ushindi katika mchezo wa fainali dhidi ya Ufaransa
Comments
Post a Comment