STRAIKA Radamel Falcao amefanikiwa kufunga bao lake la kwanza tangu aliporejea Monaco, lakini bao hilo halikuwazuia kuambulia kupata kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Fenerbahce.
Baada ya kushindwa kupata mafanikio wakati akikipiga kwa mkopo katika timu za Manchester United na Chelsea, Falcao ameamua kurejea kwa vinara hao wa Ligue 1 ambapo mkataba wake bado una miaka miwili.
Katika mchezo huo wa usiku wa kuamkia jana ulipogwa kwenye uwanja wa Sukuru Saaracogru, staa huyo mwenye umri wa miaka 30 alipangwa kikosi cha kwanza katika safu ya ushambuliaji na akaweza kuyatumia vizuri makosa yaliyofanywa na mabeki wa timu pinzani.
Bao hilo la kipindi cha kwanza cha Falcao lilifungwa na mchezaji Emmanuel Emenike, lakini kwa mara nyingine tena staa huyo wa zamani wa timu ya Westham akaihakikishia ushindi timu yake kutoka Uturuki.
Comments
Post a Comment