PSG YAANZA KUTETA NA JAMES RODRIGUEZ



PSG YAANZA KUTETA NA JAMES RODRIGUEZ
MIAMBA ya soka nchini Ufaransa, klabu ya Paris Saint-Germain ipo kwenye mazungumzo na kiungo mshambuliaji wa Real Madrid, James Rodriguez.

Rodriguez amehusishwa katika tetesi za kutua Manchester United ndani ya wiki kadhaa, lakini taarifa zilizoibuka upya ni kwamba mchezaji huyo anakaribia kutua kwenye kikosi kilicho chini ya kocha Unai Emery katika siku za hivi karibuni.

Wakati huohuo, klabu hiyo imefanikiwa kumnasa mlinzi wa klabu ya Bruges ya Ubelgiji, Thomas Meunier.  


Uhamisho wa mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 24, ulitangazwa rasmi wikiendi iliyopita.


Comments