STRAIKA wa matajiri wa Stanford Bridge, Pedro amesisitiza azma yake ya kubaki Chelsea licha ya kuwepo kwa taarifa kwamba anajipanga kwa ajili ya kurejea Hispania.
Pedro alijiunga na The Blues akitokea Barcelona kwa dau la pauni mil 21.4 lakini taarifa za sasa hivi zinasema ana mpango wa kuondoka katika Ligi ya Primer.
Klabu ya Atletico Madrid imekuwa ikitajwa katika orodha ya timu zinazomwania straika huyo mwenye umri wa miaka 28.
Tetesi hizo zinatokana na hatua ya Jose Morinho kutemwa na matajiri hao ambapo bosi huyo Mreno ndiye aliyemleta Pedro Darajani.
Ingawa mkataba wa Pedro wa miaka minne umebakiza miezi minne tu lakini anamini kuwa ana nafasi kubwa ya kuongeza mkataba chini ya kocha wa mpito wa Chelsea, Antonio Conte.
Akinukuliwa Pedro amesema: "Nina miezi minne kabla ya kumaliza mkataba wangu lakini hilo halinipi presha kwa sababu nina imani nitasalia hapa."
"Nina furaha nikiwa hapa. Nayazungumza haya kwa imani ya moyoni. Ninajivunia kuwa katika klabu kubwa."
"Nina furaha na mashabiki wa timu hii. Ingawa ni kweli kuwa hali ya mambo hapa si shwari hata kidogo, lakini kwa pamoja tunaweza tukaipandisha timu kutoka hapa."
"Ninaamini kwamba kocha Antonio Conte ni kati ya makocha wazuri na klabu ina matarajio makubwa kwake. Ninajisikia vizuri."
Comments
Post a Comment