Arsenal inakaribia kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Japan Takuma Asano baada kufikia makubaliano na klabu yake ya Sanfrecce Hiroshima.
Takuma Asano mwenye umri wa miaka 21 anakwenda Emirates na kufanya idadi ya wachezaji wa Kijapan kutumikia Arsenal kufikia watatu baada ya Junichi Inamoto na Ryo Miyaichi.
Klabu kadhaa zilikuwa zikiwania saini ya Asano lakini Arsenal imeshinda vita baada ya kufikia makubaliano na klabu ya Sanfrecce Hiroshima.
Mshambuliaji huyo aliyeichezea Japan mechi nne na kuifungia bao moja, anachukuliwa kama hazina ya baadae ya Arsenal na huenda akatolewa kwa mkopo msimu ujao.
Arsenal imekubali dili la kumsajili nyota wa kimataifa wa Japan Takuma Asano kutoka Sanfrecce Hiroshima
Mshambuliaji huyu anachukuliwa kama moja ya hazina ya kocha Arsene Wenger na anaweza kutolewa kwa mkopo msimu ujao.
Comments
Post a Comment