MOURINHO: NAFASI YA RASHFORD BADO IPO PALEPALE MANCHESTER UNITED



MOURINHO: NAFASI YA RASHFORD BADO IPO PALEPALE MANCHESTER UNITED
SIKU mbili baada ya kuinasa saini ya mshambuliaji mkongwe wa Sweden, Zlatan Ibrahimovic, kocha Jose Mourinho amesema kuwa pamoja na usajili huo, nafasi ya mshambuliaji kinda, Marcus Rashford bado ipo palepale Old Trafford.

 Kocha huyo aliyerejesha matumaini kwa mashabiki wa Manchester United, alisema atawatumia wachezaji wote kwa kuwa anajua mfumo wa klabu hiyo.

Mourinho anayesifika kwa kutumia mfumo wa mshambuliaji mmoja mbele, amesema aina ya uchezaji wa Marcus Rashford na Zlatan Ibrahimovic inafanana.

"Naweza kusema Rashford na Ibrahimovic ni washambuliaji wa kweli ambao wanajua kupambana kwa muda wote wa mchezo, nataraji kuwatumia wote," alisema.

Alisema anadhani nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney na Anthony Martial watatumika kama washambuliaji wasaidizi.

Mourinho alielezea kukerwa nay ale yanayozungumzwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba amedhamiria kukiua kipaji cha Rashford mwenye miaka 18 kwa kumsajili nguli huyo mwenye miaka 34.

Zlatan ametua Old Trafford akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia PSG ya Ufaransa na aliwaambia mashabiki kuwa yeye na Mourinho ni watu wa mataji.


"Alisema pamoja na umri wake kuanza kwenda, lakini bado ana uwezo wa kutosha kuweza kuisaidia timu hiyo ambayo kwa misimu miwili imekuwa ikiyumbayumba na kuwaumiza mashabiki wake," alisema.


Comments