Manchester United ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa kiungo mchezeshaji wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan.
Borussia Dortmund imefichua kupitia mtandao wao rasmi kuwa kiungo huyo anaondoka na wanamtakia kila la kheri.
Klabu hiyo imesema haikuwa na namna nyingine zaidi ya kumuuza Mkhitaryan kwa kuhofia kumpoteza bure msimu ujao.
"Borussia Dortmund na kiungo Henrikh Mkhitaryan (27) wanaachana rasmi kiangazi hiki," alisema mtendaji mkuu wa klabu hiyo Hans-Joachim Watzke.
Nahodha huyo wa kimataifa wa Armenia ataungana na Zlatan Ibrahimovic ndani ya Old Trafford na kuwa usajili wa tatu wa Jose Mourinho kiangazi hiki.
United inatarajiwa kulipa pauni milioni 26 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake Borussia Dortmund.
Mkhitaryan ambaye bado hajakifikia makubaliano kuhusu maslahi yake binafsi na Manchester United, atahitajika kufuzu vipimo vya afya kabla usajili wake haujathibitishwa rasmi.
Pia atahitaji kupata kibali cha kufanya kazi England kabla dirisha la usajili la Premier League halijafungwa.
Nyota wa Borussia Dortmund Henrikh Mkhitaryan amekamilisha usajili wa kujiunga na Manchester United
Borussia Dortmund imemuuza Henrikh Mkhitaryan kwa pauni milioni 26 kwenda Manchester United
Comments
Post a Comment