- Get link
- X
- Other Apps
MANCHESTER UNITED inakaribia kufanya usajili wa kiungo wake zamani Paul Pogba kwa ada ya pauni milioni 80 ambayo itakuwa ni rekodi mpya ya klabu.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, tayari yuko mazungumzoni na Manchester United ambapo inaaminika dili lake la kurejea Old Trafford litakamilika pindi tu michuano ya Euro 2016 itakapomalizika.
Pogba, 23, alikuwa kwenye rada ya Real Madrid lakini sasa anataka kujumuika na Jose Mourinho katika klabu ambayo ilimwachia aondoke bure mwaka 2012.
Juventus haina mpango wa kumwachia mkali huyo kwa pesa iliyo chini ya pauni milioni 82.8, lakini wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola anatajwa kuwa kwenye mipango mizito ya kuhakikisha kuwa Pobga anatua Old Trafford.
Gazeti la L'Equipe la Ufaransa linasema Mourinho anakaribia kumnasa Pobga na kwamba mchezaji huyo atakuwa nguzo muhimu katika mfumo wa 4-3-3 utakaotumiwa na Manchester United msimu ujao.
Mourinho anataka Pogba na nahodha Wayne Rooney wazungushe dimba la kati, Zlatan Ibrahimovic akiwa mashambuliaji pekee huku Anthony Martial na Henrikh Mkhitaryan wakicheza pembeni.
- Get link
- X
- Other Apps

Comments
Post a Comment