KLABU ya Manchester City imewaruhusu kuondoka wachezaji wake wakongwe, Martin Demichelis na Richard Wright, baada ya mikataba yao kufikia ukingoni.
Nyota wa kimataifa wa Argentina, Demichelis aliletwa kwenye klabu hiyo mwaka 2013 na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, manuel Pellegrini ambaye aliwahi kucheza chini yake wakati akiinoa timu ya Malaga.
Katika msimu wake wa kwanza akiwa na klabu hiyo ya Etihad, aliisaidia kutwaa ubingwa wa Ligi ikiwa ni baada ya kucheza mechi 35 katika mashindano yote.
Hata hivyo, misimu iliyofuata haikuzaa matunda na huku kikosi hicho kikifanikiwa kutwaa ubingwa mara moja ndani ya miaka miwli na huku nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kwa Demichelis ikiwa ngumu baada ya kusajiliwa mastaa wengine, Nicolas Otamendi na Eliaquim Mangala.
Kwa upande wake, Wright ameshatangaza kustaafu kucheza soka baada ya kushindwa kuingia uwanjani katika kipindi cha miaka minne aliyokaa Man City.
Katika kipindi cha uchezaji wake, staa huyo mwenye umri wa miaka 38, amewahi kucheza kikosi cha England mara mbili na pia amewahi kuzichezea timu za Ipswich Town Arsenal na Everton.
"Kila mmoja Manchester City anawatakia kila la kheri, Martin na Richard katika safari yao na anawashukuru kwa huduma yao," ilieleza taarifa iliyotumwa kwenye tovuti ya Man City.
Comments
Post a Comment