LIVERPOOL YAJIANDAA KUIVAA EVERTON KWANIA SAINI YA AXEL WITSEL



LIVERPOOL YAJIANDAA KUIVAA EVERTON KWANIA SAINI YA AXEL WITSEL
TIMU ya Liverpool inaripotiwa kuwa katika maandalizi ya kuivaa Everton katika mbio za kumwania staa Axel Witsel, baada ya waliokuwa wakimfukuzia awali, Gregorz Krychowiak kunaswa na mabingwa wa Ufaransa, Pais Saint-Germain.

Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Star, kwa muda mrefu Reds walikuwa wakimfukuzia kiungo huyo mkabaji ambaye ameonyesha kiwango kizuri katika fainali za michuano ya mataifa Ulaya, lakini nyota huyo kwa sasa ameamua kumfuata kocha wake, Unai Emery kutoka Seville ili wakafanye kazi pamoja kwa matajiri hao wa Ufaransa.


Gazeti hilo liliripoti kwamba hali hiyo inamuacha kocha Klopp akiwa na nafasi ya kujaza na hivyo anaona Witsel ndie chaguo lake linguine lililopo kwenye orodha yake.


Comments