LIONEL MESSI, BABA YAKE KUKATA RUFAA KUPINGA ADHABU YA KIFUNGO



LIONEL MESSI, BABA YAKE KUKATA RUFAA KUPINGA ADHABU YA KIFUNGO
WAKILI wa staa Lionel Messi na baba yake Jorge, amesema kuwa watakata rufaa kupinga adhabu ya kifungo cha miezi 21 walichopewa wateja wake baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la ukwepaji kodi.

Hatua hiyo imekuja baada ya nyota huyo wa Barcelona, Messi kutiwa hatiani na mahakama ya Hispania kwa kosa la kukwepa kodi ya euro mil 4.1 katika kipindi cha kati ya mwaka 2007 na 2009.

Hata hivyo, inaonekana Messi hawezi kutumikia kifungo hicho kutokana na kwamba kesi hiyo ishaunguruma kwa muda wa miaka miwili na kwa mujibu wa sheria za Hispania, adhabu hiyo inaweza ikafutwa.


Kutokana na hali hiyo, wakili wa Messi amesema kuwa anavyoona kesi hiyo ni ya uzushi na huku akisema, wateja wake hawana hatia na akasema kuwa ataendelea kupambana na uamuzi huo.


Comments