LEO NI MWAKA MMOJA WA KIFO CHA BANZA STONE: JIKUMBUSHE MAZISHI YAKE YALIVYOKUWA



LEO NI MWAKA MMOJA WA KIFO CHA BANZA STONE: JIKUMBUSHE MAZISHI YAKE YALIVYOKUWA

TAREHE kama ya leo mwaka jana, tasnia ya muziki wa dansi Tanzania ilipata pigo kubwa baada ya mwimbaji na mtunzi nyota Ramadhan Masanja "Banza Stone" kufariki dunia.

Banza aliyeng'ara zaidi na bendi za Twanga Pepeta, TOT, Bambino Sound na Extra Bongo, akazikwa kwenye makaburi ya Sinza jijini Dar es Salaam siku moja baadae.

Jikumbushe mazishi yake yalivyofanyika.
 Msafara wa kuelekea msikitini 
 Steve Nyerere mbunge mtarajiwa wa Kinondoni (wa pili kulia) akishiriki msiba wa Banza 
 Mwili unatolewa msikitini tayari kwa kuanza safari ya kuelekea makaburini
 Juma Nature (kushoto) akishiriki kubeba jeneza la Banza
 Hili ndio kaburi la Banza Stone
 Umati wa watu tayari ukiwa umewasili makaburini
 Katikati mwenyr fulana nyeusi ni meneja wa Mashauzi Classic Ismail Sumaragar
 Watu wakiwa makaburini wakiusubiri mwili wa Banza
 Ndugu wa warehemu wakiwa ndani ya kaburi tayari kwa kuupokea mwili wa Banza
 Mwili wa Banza ukiwasili makaburini
 Harakati za kuushusha mwili wa Banza zinaendelea
 Mwili wa Banza sasa unaingizwa kaburini
 Mwili wa Banza tayari umeingizwa kaburini
 Mwenye fulana nyeusi ni Hajji mtoto wa Banza akingalia mazishi ya baba yake yanavyoendelea
 Kushoto ni Hajji Masanja na katikati ni meneja wa Twanga Pepeta Hassan Rehani
 Mwimbaji Dogo Rama wa Twanga Pepeta akishiriki mazishi ya Banza
 Mwenye kofia nyeupe ni Juma Nature akishiriki kufukia kaburi la Banza
 Mazishi  ya Banza yamekamilika
 Ni wasaa wa kupata dua kwa wanafamilia na watu wa karibu wa marehemu
Ndugu wa Banza Stone wakifanya dua baada ya washiriki wengine kuondoka makaburini





Comments