KOCHA mpya wa klabu ya Southampton, Claude Puel amedhamiria kutoa kiasi cha pauni mil 12. 5 kumnyakua mlinzi wa klabu ya Lille, Djibril Sidibe.
Puel anataka kukamilisha usajili wake wa kwanza kwa kumnasa kiraka Sidibe ambaye ana uwezo wa kucheza kama beki wa kulia au kushoto.
Sidibe amekuwa na nia ya kutua katika Ligi Kuu ya England kwa ajili ya kusaka nafasi ya kuitwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa, baada ya kuikosa nafasi hiyo mwaka huu.
Southampton itakabiliwa na upinzani kutoka kwa klabu za Monaco na Paris Saint-Germain zinazowania saini ya mlinzi huyo pia.
Comments
Post a Comment