KOCHA aliyeondoka              katika kikosi cha timu ya taifa ya Hispania, Vecente Del              Bosque amesema kwamba alituma ujumbe kwa kila mchezaji wake              ili kueleza kuondoka kwake baada ya kutolewa katika fainali              za Mataifa ya Ulaya "Euro 2016" isipokuwa mlinda mlango wao,              Iker Casillas.
        Juzi Del Busque              alitangaza kuachia ngazi baada ya kushuhudia Hispania              ikivuliwa ubingwa wa Ulaya na Italia katika hatua ya 16              Bora.
        Katika kipindi              cha miaka saba aliyokinoa kikosi hicho, kocha huyo mwenye              umri wa  miaka 65, alishatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia              mwaka 2010 na fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2012".
        Hata hivyo, Del              Bousque alisema kuwa uhusiano wake na Casillas kwa sasa sio              mzuri kutokana na kwamba mlinda mlango huyo anajisikia              kutokuwa na furaha kutokana na kuwa hataki kuanzia benchi              nyuma ya David de Gea.
        "Kwa wachezaji              wake anawasiliana nao vizuri, lakini kwa upande wa benchi la              ufundi ni balaa," Del Bousque aliliambia jarida la El              Larguero.
        "Na hii ndio              maana sikutuma ujumbe kwa Cassillas. Anajisikia vibaya              kwangu mimi na si kwangu mimi tu hata kwa kocha wa viungo,              Javier Minano, kocha msaidizi, Toni Grande. Kwa wengine hana              shida lakini hasira zake ni kwetu," aliongeza kocha huyo.
        
Comments
Post a Comment