KOCHA Mauricio              Pochettino amethibitisha kwamba wachezaji Federico Fazio,              Nabil Bentaleb na Alex Pirtichard msimu huu wasitarajie kuwa              sehemu ya kikosi chake cha Tottenham.
        Nyota hao watatu              wameachwa kwenye kikosi hicho na Spur ambacho wiki hii              kitacheza mechi za Kombe la mabingwa wa kimataifa dhidi ya              timu za Juventus na Atletico Madrid sambamba na straika              Clinton N'jie ambaye anahusishwa kutimkia katika timu ya              Marseille.
        Hata hivyo              Pochettino anadai kuwa N'jie ameachwa jijini London kutokana              na kuwa ni majeruhi, lakini inaonyesha Fazio, Bentaleb na              Pritchard huenda wako katika mchakato wa kusaka timu mpya.
        "N'jie ni              majeruhi yupo jijini London na hawezi kucheza," alisema              majuzi kocha huyo.
        "Hali ya              wachezaji wengine ipo wazi. Hawapo kwenye mipango yangu,"              aliongeza kocha huyo.
        
Comments
Post a Comment