KOCHA Brendan Rodgers amezikana tetesi zinazomuhusisha na kibarua cha kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya England, akisema kwamba mawazo yake yote yapo kwenye kazi yake mpya ya kuinoa Celtic.
Hadi sasa ni mwezi mmoja tangu kocha huyo wa zamani wa Liverpool aanze kuinoa klabu hiyo ya jijini Glasgow, lakimni pamoja na hilo amekuwa akitajwa kujiuzulu wakati jina lake likiongozwa kwa wanaopewa nafasi ya kuwanoa simba hao watatu.
Hata hivyo, jana Rodgers alikanusha kuwa na mpango huo wa kuondoka Parkhead, licha ya kupewa nafasi hiyo kubwa ya kuinoa England.
"Siwezi kung'oa mguu mahali hapa," alisema kocha huyo.
"Ila kwa sasa ni mazungumzo yanayotamba kwenye ulimwengu wa soka na ni lazima kuwepo na tetesi kama hizo," aliongeza kocha huyo.
Alisema kwamba kwa sasa ana kibarua ambacho alikuwa akikiota na anaongoza kikosi ambacho alikuwa akikiunga mkono katika maisha yake yote.
Comments
Post a Comment