KINDA GUILLERMO AOMBA KUONDOKA OLD TRAFFORD KUMKIMBIA JOSE MOURINHO



KINDA GUILLERMO AOMBA KUONDOKA OLD TRAFFORD KUMKIMBIA JOSE MOURINHO

MLINZI kinda wa Manchester United, Guillermo Varela ameamua kumkimbia kocha mpya wa timu hiyo, Jose Mourinho kwa kuomba kuondoka kwa mkopo kwenda kuitumikia Eintracht Frankfurt ya Ujerumani.

Taarifa ambayo hadi mapemajana ilikuwa haijathibitishwa, ilisema kuwa Manchester United imeridhia kumuachia mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alitumiwa na kocha Louis Van Gaal katika mechi.

Varela inaaminika kuwa ni sehemu tu ya wachezaji wengi ambao kuna uwezekano wakaondoka kukwepa kufanya kazi na Mourinho ambaye amekuwa hatabiriki.


Kiungo mahiri wa Hispania, Juan Mata alikuwa ni kati ya wachezaji wa kwanza waliobainisha kuwa hawatafanya kazi na Jose Mourinho ambaye alimpiga bei kiungo uyo mara tu alipotua Chelsea na sasa amekutana nae Old Trafford.


Comments