KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ametaja kilichomfanya kumrejesha nyumbani nyota wake Mamadou Sakho katika ziara yake nchini Marekani.
Amesema kwamba bado ana mazungumzo ya kina na nyota huyo ambaye alikuwa amefungiwa kwa matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni kutokana na kuwa ameshafanya makosa mara tatu tangu amalize adhabu hiyo.
Akizungumza juzi Mjerumani huyo alisema kwamba tangu nyota huyo afutiwe mashitaka, ameshafanya makosa kadhaa na hivyo anahitaji kukaa nae ili aweze kunusuru kibarua chake.
"Hivi karibuni kidogo akose ndege wakati Liverpool tukiondoka kwenda San Francisco, alikuwa haji mazoezini na amekuwa akichelewa kwenye chakula cha wachezaji," alisema Klopp.
"Kwa hapa najenga timu mpya na mwanzo wetu ni hapa. Nadhani italeta maana kama aakirejea nyumbani Liverpool," aliongeza kocha huyo.
Alisema kwamba katika timu hiyo wana kanuni na sheria ambazo zinatakiwa kuheshimiwa na kwamba kama kuna mtu ambaye hataki kuziheshimu atamchukulia hatua.
Comments
Post a Comment