KOCHA mpya wa Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kwa kile kilichomfanya kumsajili straika wake aliyemsajili msimu huu, Zlatan Ibrahimovic akisema kuwa ana mambo matatu yanayomfanya ajivune.
Kocha huyo raia wa Ureno amefanikiwa kumnasa nyota huyo wa zamani wa timu za Barcelona, AC Milan na Paris Sain-Germain baada ya staa huyo mwenye umri wa miaka 34 kuamua kuwatema mabingwa hao wa Ufaransa.
Wawili hao pia wamewahi kuwa karibu katika kipindi ambacho Mourinho alikuwa akiinoa Inter Milan na kocha huyo anasema kwamba raia huyo wa Sweden sio mtata bali ni mtu wa utani.
"Zlatan naweza kumzungumzia kwa maneno matatu; ni mshindi, mpikaji mabao na mchekeshaji," alisema Mourinho.
"Unatakiwa kumwelewa. Ni mtu wa utani, kama humfahamu pengine unaweza kumfikiria vingine," aliongeza kocha huyo.
Alisema kutokana na kuwa ni kijana mwenye utani, anaweza kusema kuwa anajivunia kwa kumpata.
Comments
Post a Comment