STAA mpya wa Liverpool, Joel Matip, amesema kwamba kutokana na michuano ya Ligi Kuu England, inataka mchezaji awe fiti, kwa hiyo mpango wake ni kwenda kujifua gym kabla ya msimu huu mpya kuanza.
Beki huyo mpya wa kati ambaye amejiunga na klabu hiyo ya anfield akitokea Schalke, amesema juzi kwamba bado kuna mambo mengi ya kufanya katika mwili wake ili kuuweka sawa kabla ya Ligi hiyo kuanza.
Mbali na kujifua gym kwa ajili ya Ligi hiyo itakayoanza kutimua vumbi Agosti 13, mwaka huu, matip mwenye umri wa miaka 24, pia mipango yake mingine ni kuhakikisha anafikia kiwango cha hali ya juu.
"Nipo tayari kwa ajili ya soka la Uingereza, lakini kuna mambo mengi ya kufanya katika mwili wangu," staa huyo aliiambia tovuti ya klabu katika siku yake ya kwanza ya mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao.
"Hii ni Ligi tofauti hivyo ni lazima kuna kitu cha kufanya katika mwili wangu ili niweze kiucheza mahali hapa na ukiwa ni mwili wenye nguvu inatosha kucheza katika Ligi hii," aliongeza staa huyo.
Comments
Post a Comment