KIUNGO wa Arsenal, Jack Wilshere amempongeza staa Granit Xhaka kwa Mswisi huyo kuamua kuitema Borussia Monchengladbach na kujiunga na Arsenal na akasema kwamba haoni kama kutakuwepo na shida kucheza naye kwenye safu ya kiungo.
Hivi karibuni Xhaka alijiunga na wachezaji wenzake baada ya kutoka kwenye mapumziko waliyopewa baada ya kumalizika fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2016" alipokuwa na timu ya taifa ya Uswisi na Wilshere anasema kwamba staa huyo anatarajiwa kuwa tegemeo kwenye klabu hiyo ya Emirates.
"Niliwahi kucheza dhidi yake wakati wa ngazi za timu za vijana nikiwa na England na vilevile nikiwa na kikosi cha kwanza nikiwa na England, hivyo namfahamu vyema," Wilshere aliiambia tovuti ya klabu hiyo ya Arsenal.
"Mara zote huwa nafahamu kuwa ni mchezaji mzuri, ana nguvu na amejaaliwa mguu mzuri wa kushoto," aliongeza nyota huyo.
Comments
Post a Comment