Kwa dakika 45 alizocheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Wigan, kiungo Henrikh Mkhitaryan aliwapa mashabiki wa Manchester United kitu roho inataka kwa kutandaza soka bab kubwa.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa kwa pauni milioni 26 kutoka Borussia Dortmund akathibitisha thamani yake kabla ya kupumzishwa kipindi cha pili na nafasi yake kuchukuliwa na Juan Mata.
Mashabiki 7000 wa Manchester United waliosafiri kwenda Wigan wakashuhudia nyota huyo wa kimataifa wa Armenia akionyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, chenga za uhakika na pasi zenye macho.
Mchezaji mpya wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan aling'ara kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wigan
Henrikh Mkhitaryan akikumbana na Emyr Huws
Henrikh Mkhitaryan akiwachambua mabeki wawili wa Wigan
Kocha mpya wa Manchester United Jose Mourinho akionyesha ishara ya kukubali mavitu ya Henrikh Mkhitaryan
Comments
Post a Comment