Mikel Arteta amethibitisha kutundika daluga na kuweka wazi kuwa anakwenda kuungana na benchi la ufundi la Manchester City chini ya Pep Guardiola.
Nahodha huyo wa zamani wa Arsenal ametoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa muda wake kama mchezaji umefika ukingoni na anakwenda kufanya kazi na Guardiola.
"Kufutatia tetesi nyingi za vyombo vya habari juu ya hatma yangu, sasa ninathibitisha kuwa naondoka Arsenal na kwenda Manchester City kama sehemu ya benchi la ufundi," aliandika Arteta.
Mikel Arteta amethibitisha kutundika daluga na kwenda kuwa kocha msaidizi Manchester City
Hapa ilikuwa ni katika mchezo wa mwisho wa Arteta kwa Arsenal mwezi Mei dhidi ya Aston Villa ambapo alibubujikwa na machozi baada ya mpira kumalizika
Arteta anakwenda kuwa msaidizi wa Pep Guardiola
Comments
Post a Comment