HATIMAYE MANCHESTER UNITED YAKAMILISHA USAJILI WA PAUL POBGA KWA PAUNI MIL 100 ...atavaa jezi namba sita, mshahara pauni 290,000 kwa wiki
Paul Pogba anatarajiwa kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Manchester United kufuatia kukamilika kwa uhamisho wake wa rekodi ya dunia wa pauni milioni 100.
Taratibu za usajili wa Pobga unaomfanya arejee Old Trafford kwa mara ya pili, ulikamilishwa Alhamisi usiku.
Baada ya wiki kadhaa za majadialiano ya kina, United imekubaliana na ada ya Juventus kukamilisha usajili wa nne wa Jose Mourinho kiangazi hiki.
Pobga amekamilisha vipimo vya afya huko Los Angeles na atavaa jezi namba 6 Manchester United.
Dili hilo la usajili wa Pobga mwenye umri wa miaka 23, limekamilika baada ya wakala wake Mino Raiola kufanya maongezi na mawakili na maofisa wa Juventus Alhamsi mchana huko Turin.
Hii inamaanisha kuwa mchezaji huyo aliyeondoka Old Trafford kama mchezaji huru mwaka 2012, anarejea akiwa mchezaji ghali anayevunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa pauni milioni 40.
Rekodi ya Uingereza ilikuwa inashikiliwa na Angel di Maria aliyenunuliwa na Manchester United kwa pauni milioni 60 kutoka Real Madrid.
United na Juventus zimekubaliana ada ya wakala Riola ambaye atahitaji asilimia 20 ya dili la Pobga.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa, anatarajiwa kulipwa mshahara wa pauni 290,000 kwa wiki.
Comments
Post a Comment