BAADA ya klabu mbalimbali kuwania saini ya nyota wa Argentina, Gonzalo Higuain aliyekuwa akihudumu SSC Napoli, hatimaye nyota huyo ameamua kubaki katika serie A lakini akijiunga na miamba ya kandanda, Juventus kwa kitita cha euro mil 94.
Hatua hiyo imezifanya klabu za Liverpool, Arsenal na Atletico Madrid kusimama kumfukuzia nyota huyo mwenye miaka 28.
Aidha hatua ya Juventus kumnunua inatafsiriwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa huenda wapo njiani kumwachia kiungo wao, Paul Pogba atue Manchester United huku wakimtaka kiungo wa Axel Witsel wa Zenit kuziba pengo hilo.
Nyota huyo aliyekwenda nchini Hispania juma moja lililopita kwa ajili ya kupima afya yake kwa ajili ya kujiunga na Biaconneri.
Higuain amesaini mkataba wa miaka minne ya kuitumikia miamba hiyo ya serie A akizama hapo akiwa mchezaji bora wa msimu wa 2015/16.
Msimu uliopita nyota huyo wa zamani wa Real Madrid amefunga mabao 36 katika serie A na kuiwezesha kucheza Ligi ya mabingwa msimu ujao.
Hata hivyo, mashabiki wa Napoli wamepania kumtendea visivyo Higuain pale miamba hiyo itakapokutana Oktoba 30, mwaka huu kwenye mchezo wa serie A msimu huu.
Comments
Post a Comment