KOCHA mpya wa Manchester City, Pep Guardiola amesisitiza kuwa jukumu lake la kwanza ndani ya klabu hiyo ni kuhakikisha anarudisha umoja na kuifanya icheze soka la kuvutia.
Mhispania huyo alitambulishwa rasmi mbele ya maelfu ya mashabiki waliokuwepo kwenye academia ya klabu hiyo wikiendi iliyopita na kuweka wazi mikakati yake.
"Lengo la kwanza ni kurudisha umoja na ushirikiano pamoja na kuifanya timu icheze soka zuri, baada ya hapo nitajaribu
kushinda mchezo mmoja na utakaofuata na mwingine tena."
"Ninachokitaka kutoka kwa mashabiki wetu na wale wanaopenda soka, wafurahie kile tutakachokifanya baada ya hapo tutajua tupo kwenye gazi ipi. Labda tutashinda mataji, lakini kawa watu hawatajivunia kwa kile tunachokifanya basi tutakuwa hatujafanya lolote."
"Ni changamoto ndio maana nipo hapa, lakini sitoweza kufanya hilo peke yangu. Tunawahitaji mashabiki wetu kwani bila wao haitawezekana."
"Ndani ya muda mfupi tutajaribu kutengeneza ushirikiano ndani ya timu. Tunahitaji kutengeneza kitu cha muhimu zaidi baina yetu. Hicho ndicho kitu cha muhimu na mengine yatafuata."
Comments
Post a Comment