STAA wa timu ya taifa Italia, Graziano Pelle amewaangukia mashabiki kwa kukosa penati katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2016" ambao walifungwa na Ujerumani.
Staa huyo wa Southampton ni mmoja kati ya wachezaji wanne ambao walikosa penati ambao walikosa penati baada ya mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya muda wa dakika 120 na huku wenzake, Simone Zaza, Leonardo Bonucci na Matteo Darmian, nao walishindwa kutumbukiza mipira yao kimiani.
Pelle alikuwa akishutumiwa kwa ishara aliyoionyesha kwa mlinda mlango wa Ujerumani, Manuel Neuer na sasa nyota huyo ameamua kuomba radhi.
"Sio muhimu kwangu mimi. Kwangu mashindano haya ni mazuri kwa Italia. Nasikitika sana na ningependa kuomba radhi kwa raia wote wa Italia. Ninaomba kusema samahani kwa wachezaji wenzangu, kwa kocha, kwa mashabiki na kwa kila mmoja ambaye ananitakia mema," Pelle aliwaambia waandishi wa habari.
"Nilikuwa na kazi moja ambayo ilikuwa ni kupiga penati na kufunga. Ningeweza kujisifu kama ningeweza kufanya hivyo. Sikuwa kitu chochote wakati nilipowasili katika fainali hizo za Euro na bado mimi sio kitu kwa sasa. Lakini mara zote nimekuwa nikijitolea kwa kila kitu nikiwa katika jezi ya Italia."
Comments
Post a Comment