FERGUSON AUNGA NA MOURINHO KUMSALITI GIGGS UNITED


FERGUSON AUNGA NA MOURINHO KUMSALITI GIGGS UNITED

Bildnummer: 12959187 Datum: 05.03.2013 Copyright:              imago/Sportimage Jose Mourinho manager of Real Madrid shakes              the hand of Sir Alex Ferguson manager of Manchester United              and leaves the pitch minutes before the end - UEFA CHAMPIONS              LEAGUE - ROUND OF 16 - Manchester Utd vs Real Madrid - Old              Trafford Stadium - Manchester - 05/03/13 - Picture Simon              Bellis/Sportimage- PUBLICATIONxNOTxINxUK ; Fussball              Champions League 2012 Achtelfinale Manchester United FC ManU              Real Madrid xdp x0x 2013 hoch 2013 football Manchester Utd              Real Madrid UEFA UCL Champions League Image number 12959187              date 05 03 2013 Copyright imago Jose Mourinho Manager of              Real Madrid Shakes The Hand of Sir Alex Ferguson Manager of              Manchester United and leaves The Pitch Minutes Before The              End UEFA Champions League Round of 16 Manchester Utd vs Real              Madrid Old Trafford Stage Manchester 05 03 13 Picture Simon              Bellis PUBLICATIONxNOTxINxUK Football Champions League 2012              Eighth finals Manchester United FC ManU Real Madrid x0x 2013              vertical 2013 Football Manchester Utd Real Madrid UEFA UCL              Champions League

Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ametetea uamuzi wa Jose Mourinho kutomjumuisha Ryan Giggs kwenye timu yake ya benchi la ufundi la klabu hiyo.

Giggs, ambaye ni mchezaji aliyedumu United kwa kipindi kirefu zaidi, na aliyekuwa meneja msaidizi wa Louis van Gaal, ametangaza kuondoka Old Trafford mwishoni mwa wiki hii, na kukamilisha miaka yake 29 aliyodumu klabuni hapo kama kocha na mchezaji.

Ferguson anaamini kwamba Mourinho alikuwa sahihi kabisa kumleta msaidizi wake anayemwamini kwa kiasi kikubwa Rui Fara, ambaye amekuwa akifanya naye kazi kokote aendapo.

"Unatakiwa uwe na msaidizi wako ambaye umekuwa ukimwamini kwenye maisha yako yote," Ferguson amesema.

"Wakati nilipokuja Man United, nilimleta Archie Knox, kwasabau alikuwa mtu mwenye thamani sana kwangu.

"Nilimwamini kwa asilimia 100, Jose Mourinho amekuwa na msaidizi wake kwa miaka nenda-rudi, kitu ambacho ni kizuri kwake kwa kudumu na mtu mmoja.

Kama Jose asingekuwa na msaidizi, nafahamu fika kwamba angemchukua Ryan.

"Ni muda mwafaka sasa kwa Ryan kusimama mwenyewe, aondoke pale na kutafuta changamoto mpya.

Ferguson,ambaye alistaafu kuifundisha United mwaka 2013 baada ya kudumu kwa miaka 26, amesema Giggs ana kila sababu ya kutafuta timu kubwa na kuweza kuifundisha kwa sababu anao uwezo.

"Nadhani kwa sasa ameshakuwa tayari kuweza kufundisha timu yoyote na kimsingi ana ubora wote unaostahili," Ferguson aliongeza.

"Hatakiwi kwenda kwenye klabu ambayo inafukuza makocha kila baada ya dakika mbili." alimalizia.



Comments