FABREGAS AMPONDA MOURINHO NA KUSEMA SIO KITU KWAKE BALI WENGER NDIO MPANGO MZIMA



FABREGAS AMPONDA MOURINHO NA KUSEMA SIO KITU KWAKE BALI WENGER NDIO MPANGO MZIMA
KIUNGO wa Chelsea, Cesc Fabregas ni kama kampotezea kocha wake wa zamani, Jose Mourinho baada ya kusema kuwa Arsenal wenger ndie kocha muhimu katika kibarua chake na wala sio Mreno huyo.

Kiungo huyo raia wa Hispania alitumia muda wa miaka minane akiwa arsenal kabla ya kwenda kujiunga na klabu iliyomlea ya Barcelona.

Baadae Fabregas mwenye umri wa miaka 29 alivutwa na Jose Mourinho Chelsea mwaka 2014 na mashabiki wa Arsenal wakakasirika kujiunga na mahasimu wao kwenye michuano ya Ligi Kuu England.

Kiungo huyo anasemekana kuwa na bahati ya kucheza chini ya makocha wazuri kama Mourinho na Pep Guardiola, lakini Mhispania huyo anamsifu Wenger kuwa ndie kocha muhimu katika kibarua chake.

"Kwa ujumla Arsene Wenge ndio kocha bora kwangu kwasababu alikuwa akinipa nafasi ya kweli ambayo kila mmoja huwa anaitaka na kuihitaji," alisema Fabregas katika mahojiano na mtandao wa Four Four Two.

"Baada ya hilo, hapo ndipo unapoweza kuthibitisha kama ni mtu safi ama mbaya, hilo lipo juu yako. Lakini kwangu mimi alikuwa akinipa nafasi," aliongeza nyota huyo.


Alisema kwamba Mfaransa huyo alimchukua wakati akiwa na umri wa miaka 16 na akafanya kuwa mchezaji bora, hivyo mara zote amekuwa akimchukulia kama baba yake wa pili.


Comments