EVERTON MBIONI KUMNASA MLINZI LAMINE KONE WA SUNDRELAND



EVERTON MBIONI KUMNASA MLINZI LAMINE KONE WA SUNDRELAND
KLABU ya Everton ipo mbioni kumdaka mlinzi wa kati wa Sunderland, Lamine Kone kwa kitita cha pauni mil 15 endapo John Stones atatimkia Manchester City.

Kocha Ronald Koeman anamtaka Kone ambaye ana miaka 27, akisaidia Sunderland iliyokuwa chini ya Sam Allardyce ili isiweze kushushwa daraja.

Nyota huyo wa Ivory Coast amecheza mechi 15 za Ligi Kuu England (EPL) na kufunga mabao mawili dhidi ya Everton walipokuwa katika harakati za kujinasua na mkasa wa kushuka daraja msimu uliopita.

Kone alijiunga Januari mwaka huu akitokea Lorient kwa kitita cha pauni mil 6 ambapo hadi sasa anawaniwa na Leicester City na Westbrom.

Hata hivyo, Everton wapo katika mazungumzo na klabu ya Napoli kuhusu Kalidou Koulibaly ambaye anatamani kutua Chelsea kwa kitita cha pauni mil 40.

Koeman anatrajia kuwa John Stones ataondoka klabuni hapo kwenda Manchester City kwa pauni mil 50, huku Phil Jagielka akiwa majeruhi ya nyama za paja huku Ramiro Funes Mori akijiandaa na michuano ya Olimpiki akiwa na Argentina.


Kocha mpya wa Sunderland, David Moyes alikaririwa akisema kuwa klabu hiyo ina ukata wa fedha, hivyo kumuuza nyota huyo kunaweza kutumika kupata ahueni kwa ajili ya ujenzi.


Comments