Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 katika muda wa kawaida na hadi dakika 30 za 'extra time' na ndipo hatua ya penalti tano tano ilipofuata na Ureno kutupia wavuni penalti zake zote tano huku Poland ikipoteza moja kati ya penalti nne ilizopiga.
Cristiano Ronaldo, Renato Sanches, Joao Moutinho, Nani na Ricardo Quaresma waliifungia Ureno kwenye mikwaju ya penalti wakati Robert Lewandowski, Arkadiusz Milik na Kamil Glik waliifungia Poland huku Jakub Blaszczykowski akishuhudia shuti lake likipanguliwa na kipa Rui Patricio na kufanya matokeo ya penalti yawe 5-3.
Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski aliifungia Poland bao la kuongoza dakika ya pili lakini kiungo mpya wa Bayern Munich Renato Sanches akaisawazishia Ureno kunako dakika ya 33.
Comments
Post a Comment