KOCHA Diego Simeone amesema kuwa hajali kila kinachozungumzwa juu yake kuhusu hatma yake ya Atletico Madrid baada ya mwezi uliopita kufungwa tena katika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mwezi huo uliopitwa Atletico ilijikuta ikifungwa tena katika hatua hiyo kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu na mara zote hizo ikiwa inafungwa na mahasimu wao, Real Madrid.
Baada ya mikwaju hiyo ya penati na Real Madrid katika mtanange uliopigwa mjini Milan, Simeone alisema kuwa itamlazimu kutafakari upya juu ya kibarua chake kwenye klabu hiyo ya Vicente Calderon.
Hata hivyo, jana kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, alisema kuwa katika kipindi kama hicho unaweza kusema hivyo, lakini akasema kuwa yeye bado anaitumikia Atletico.
"Nilizungumza kama hivyo na sisi Waargentina tupo kama hivyo," alisema kocha huyo jana.
Comments
Post a Comment