KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps amempongeza staa wake Antoine Griezmann na amesema kuwa anatarajia makubwa kutoka kwake katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016.
Katika mchezo wa majuzi ambao waliondoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Iceland, Griezmann aling'ara tena kipindi cha kwanza na kufunga bao jingine ambalo limekifanya kikosi chake kikutane na Ujerumani katika hatua ya nusu fainali.
Hadi sasa staa huyo wa Atletico Madrid ndie anayeongoza kwa kuziona nyavu katika mashindano hayo akiwa na mabao manne, jambo ambalo linamfanya Deschamps kumpongeza staa huyo mwenye umri wa miaka 25.
"Anaweza kuendelea kung'ara kwa muda mrefu na endapo ataendelea kuongoza kwa ufungaji itakuwa ni vizuri kwetu," alisema kocha huyo.
"Antoine alikuwa katika hali mbaya wakati alipoanza mashindano haya, hivyo alihitaji kujisimamia wakati wa siku tisa za mwanzo za mashindano haya," aliongeza kocha huyo.
Comments
Post a Comment