CRISTIANO RONALDO ATAKA AONGEZEWE MKATABA MWINGINE REAL MADRID



CRISTIANO RONALDO ATAKA AONGEZEWE MKATABA MWINGINE REAL MADRID
STRAIKA Cristiano Ronaldo anasemekana kuwa anataka kuongeza mkataba na klabu yake ya Real Madrid na ni kwamba atafanya mazungumzo kuhusu hatma yake pindi atakaporejea katika mji mkuu huo wa Hispania.

Mkataba wa sasa wa staa huyo raia wa Ureno unatarajiwa kumalizika Juni, 2018, lakini inasemekana kuwa yupo tayari kujitia kitanzi cha muda mrefu.

"Nimeshazungumza na rais Florentino Perez kwa njia ya simu na wakati nitakaporejea mjini Madrid tutazungumza kuhusu suala la kupewa mkataba mpya," staa huyo mwenye umri wa miaka 31 alikaririwa na shirika la habari la Hispania AS.

"Kwa ujumla hicho ndicho kitu ninachokihitaji," aliongeza nyota huyo katika mahojiano na shirika hilo.


Real Madrid itazianza kampeni za msimu wa 2016/17 kwa kushiriki Kombe la UEFA Super Cup dhidi ya Sevilla, mtanange ambao utapigwa Agosti 9, mwaka huu katika mji wa Trondheim, lakini Ronaldo ataikosa mechi hiyo baada ya kuongeza muda wa mapumziko kutokana na majeraha ya goti yanayomkabili aliyoyapata akiwa na timu ya taifa ya Ureno katika michuano ya Euro 2016.


Comments