NYOTA wa zamani wa Barcelona, Hristo Stoichkov amedai kuwa nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo huenda akatwaa tuzo ya Ballon d'Or kutokana na mawazo yake ya kusema kuwa Antonio Griezmann na Gareth Bale kama washindani.
Griezmann na Bale wanajiandaa kwa mechi za nusu fainali za Euro 2016 baada ya kampeni nzuri walizofanya katika klabu zao za Atletico na Real Madrid.
Mfaransa Griezmann amefunga mabao 32 katika michuano yote akiwa Atletico, timu yake ikimaliza nafasi ya tatu La Liga na kupoteza fainali Ligi ya Mabingwa kwa Real Madrid, wakati Bale akiwa amefunga mara 19 na kutoa pasi 10 za goli.
Lakini ikiwa ni wiki moja tangu alipomtaja James Rodriguez wa Real Madrid kama mchezaji wa kawaida sana, mkongwe huyo wa Bulgaria aliamua kumzungumzia mshindi mara nne wa tuzo ya Ballon d'Or, Ronaldo.
"Griezemann ni mchezaji hatari kwa kila mtu na ancheza soka matata sana," Stoichkov aliiambia radio ya Hispania Cadena Cope.
"Lakini huenda wakampa Cristiano Ronaldo tuzo hiyo tena kwa sababu ya umbile lake zuri."
Kuhusu Bale ambaye atacheza dhidi ya Ureno leo, halikadhalika nae akitarajiwa kuingia kwenye mbio za Ballon d'Or, Stoichkov alisema mchawi huyo wa soka wa Wales atakuwa miongoni mwa wanaowania tuzo hiyo iwapo Wales itatinga fainali Euro.
Comments
Post a Comment