CLAUDIO RANIERI AMTABIRIA MOURINHO MAFANIKIO KAMA YA SIR ALEX FERGUSON MAN UNITED



CLAUDIO RANIERI AMTABIRIA MOURINHO MAFANIKIO KAMA YA SIR ALEX FERGUSON MAN UNITED
KOCHA wa klabu ya Manchester City, Claudio Ranieri amemtabiria kocha mpya wa Manchester United kuwa atapata mafanikio kama aliyoyapata kocha wa zamani wa “Red Devils” hao, Sir Alex Ferguson ndani ya dimba la Old Trafford.

Akiwa na kikosi cha Leicester City, Ranieri alipewa nafasi moja kati ya 500 za kunyakua taji la Ligi Kuu England msimu uliopita na kwa kile kilichoonekana kama maajabu mapya ya soka, Leicester ilibeba taji hilo kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 132 tangu klabu hiyo ianzishwe.

Mourinho alinyakuliwa na United na kupewa mkataba wa kuinoa timu hiyo iliyokuwa chni ya Mholanzi Louis Van Gaal msimu uliopita na Ranieri anaamini Mreno huyo ana nafasi ya kufanya vizuri msimu ujao kwenye Ligi Kuu England.

“Mourinho ana uwezo wa kuwa Ferguson mpya,” alisema Ranieri.

“Atadumu United kwa miaka 26 lakini ataacha alama ya ushindi.”


Upinzani bainia ya Ranieri na Mourinho unategemewa kuwa mkali msimu ujao. Sambamba na makocha wengine waliotua England, Antonio Conte (Chelsea) na Pep Guardiola (Man City).


Comments