CRISTIANO Ronaldo amesema ameumizwa na machozi ya Lionel Messi kufuatia kutwaa ubingwa wa Copa America akiwa na Argentina na amemtaka mpinzani wake huyo kufikiria upya maamuzi yake ya kustaafu kuichezea timu ya taifa.
Mpango wa Messi kutwaa Copa ulimalizika kwa fadhaa kubwa pale Argentina ilipolala kwa mabao 3-0 dhidi ya Chile huku staa huyo wa Barcelona akikosa penati yake.
Ilikuwa ni mara ya nne kwa Messi kucheza mechi ya fainali na akatangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa muda mfupi baadae, jambo lililowasikitisha Waargentina wengi.
Messi na nyota wa Real Madrid, Ronaldo, wamekuwa wapinzani kwa miaka mingi wakiwania mataji kwenye La Liga na vita yao ya kawaida ya tuzo ya Ballon d'Or.
Lakini Ronaldo akizungumza kuelekea mechi yao ya nusu fainali akizungumza kuelekea mechi yao ya Euro 2016 akiwa na Ureno dhidi ya Wales, alisema Messi anahitajika katika soka la kimataifa na anapaswa kufikiria kubadili msimamo.
Ronaldo aliliambia gazeti la Mundo Deportivo: "Messi amechukua maamuzi mazito na watu wanapaswa kuelewa."
"Hajazoea vipigo na fadhaa wala kumaliza wa pili na kukosa penati hakukufanyi uonekane mchezaji mbovu."
"Inauma kumuona Messi anatokwa machozi na natumai atarejea kwenye timu yake ya taifa kwasababu anahitaji soka la kimataifa."
Comments
Post a Comment