CARLO ANCELOTTI AWAAHIDI SOKA LA KUVUTIA MASHABIKI WA BAYERN MUNICH



CARLO ANCELOTTI AWAAHIDI SOKA LA KUVUTIA MASHABIKI WA BAYERN MUNICH
KOCHA mpya wa miamba ya soka ya Ujerumani, Bayern Munich, Carlo Ancelotti amewaahidi mashabiki wake kuwa atakuwa na mchezo wa kuvutia na kushambulia.

Kama ilivyokuwa mtangulizi weake, Pep Guardiola, Ancelotti alianza kuzungumza Kijerumani kabla hajaendelea na Kiitaliano na Kiingereza wakati wa maswali na majibu.

Guardiola ameshinda mataji matatu ya Bundesliga kabla hajaamua kuachana na kuinoa miamba hiyo.

Ancelotti anatarajiwa kuwaletea Bayern taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na kuwa na historia nzuri akitoka kuinoa AC Milan na baadae Real Madrid.


Hata hivyo, mwenyekiti wa klabu hiyo, Karl-Heinz Rummenigge na Ancelotti hawana nia ya kupunguza wala kuongeza wachezaji.


Comments