KIPA mkongwe na              nahodha wa heshima wa Italia, Gianluigi Buffon ameibuka na              kuwajia juu wanaotaka kumlinganisha na kipa wa Ujerumani,              Manuel Neuer.
        Buffen, 38,              aliisaidia Italia kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 2006 na              anashikilia rekodi ya kuwa kipa ghali zaidi duniani alipotua              Juventus akitokea Parma kwa pauni mil 33 mwaka 2001.
        Kipa huyo ameweza              kuipa lundo la mataji Juventus tangu atue kikosini hapo              ambapo wametwaa mataji kibao ikiwemo ubingwa wa serie              mfululizo.
        Neuer ndiye              kwanza nae ameanza kuhesabu mafanikio ambapo mwaka 2014              aliipa ujerumani Kombe la Dunia, tayari ametwaa tuzo kadhaa              za akiwa na Bayern Munich.
        Lakini Buffon              ambaye amemwelezea Neurer kma kipa bora kwa sasa, amekataa              katakata kulinganisha nae kwa kiwango cha sasa.
        "Nimesema Neuer              ni zaidi yangu kwasababu bado ana nafasi ya kufikia na              kupita mafanikio yangu baadae, hilo sio jambo la kunikwaza              kuangalia mimi niko vipi."
        "Najijua              nilivyokuwa, nilivyo kwa sasa na wapi nitakuwa kwa miaka              miwili ijayo. Hii inanifanya niamini atapata mafanikio zaidi              siku zijazo," alisema.
        Alionya kuwa ni              kosa la jinai kumlinganisha na kipa huyo mwenye miaka 30              ambaye bado anakipiga.
        
Comments
Post a Comment